VP Samia: Wanawake wanahitaji elimu zaidi ya namna ya kukukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza watendaji wa Mradi wa Jukwaa la Kijani la wanawake N... thumbnail 1 summary
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza watendaji wa Mradi wa Jukwaa la Kijani la wanawake Nchini wahakikishe wanaendelea na mkakati wa kuelimisha wanawake kuhusu namna ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati anazindua mradi wa GREEN VOICES, mradi unaolenga kusaidia wanawake kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi, unaofadhiliwa na Rais wa Mfuko wa Wanawake Barani Afrika Maria Tereza Fernandes De la Vega .

Makamu wa Rais pamoja na kupongeza jitihada zinazofanywa na Jukwaa hilo katika kusaidia wanawake kupambana na mabadiliko ya Tabianchi, amesema bado upo umuhimu mkubwa kwa wanawake kuelimishwa zaidi kuhusu mabadiliko hayo kwa sababu wao ni moja ya kundi ambalo linaguswa na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo suala la ukame.

Amesema bara la Afrika linapoteza mabilioni ya dola kutokana na mabadiliko ya Tabianchi ikiwemo tatizo la ukame ambao umechangia kupunguza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kwa kiasi kikubwa pamoja na uhaba wa maji.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema nchi za Afrika bado zinakabiliwa na uhaba wa fedha,taarifa sahihi na teknolojia katika jitihada za kupambana ipasavyo na mabadiliko ya tabianchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Green Voices Tanzania uliofanyika katika hoeteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo namna ya mkaa wa karatasi unavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Mchau Windmill Ndugu Laurian Mchau wakati wa uzinduzi wa mradi wa Green Voices Tanzania .
Keki ya Muhogo.
Mkaa wa karatasi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akipata maelekezo ya namna zao la muhogo.
Mshauri na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Wanawake Barani Afrika Mhe. Getrude Mongella akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Green Voices Tanzania uliozindiliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 


Chanzo: Issa Michuzi blog, Imehaririwa na Tabianchi blog