TMA yatoa tahadhari mvua kubwa leo

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha kwa mvua kubwa inayofikia asilimia 80 kuanzia leo Jumatano usiku hadi... thumbnail 1 summary
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha kwa mvua kubwa inayofikia asilimia 80 kuanzia leo Jumatano usiku hadi kesho kutwa.
Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Jumatano Januari 10, 2018 imesema mvua hizo zitanyesha katika maeneo mengi ya ukanda wa Pwani ya Kusini ambayo ni Lindi, Mtwara na maeneo ya Morogoro Kusini.
“Vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 vinatarajiwa kuanzia Januari 10, 2018 hadi Januari 12, 2018,” imeeleza taarifa hiyo ya TMA na kuongeza;
“Hali hii inatokana na kuwepo na kuimarika kwa ukanda wa mvua (Inter Tropical Convergency Zone –ITCZ) na mgandamizo mdogo wa hewa uliopo kwenye mkondo wa bahari wa Msumbiji.”
TMA imetoa tahadhari kwa wakazi wa maeneo yaliyotajwa kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari zinazotolewa.